Mpenzi msomaji u hali gani?
Leo napenda nikufahamishe kuhusiana na uwepo wa magari tajwa hapo juu. Ni magari yenye uwezo wa kutumia mfumo mmoja baada ya mwingine. Inamaana kuna mfumo wa gesi na mfumo wa mafuta ya dizeli ama petroli. Hivyo basi unaweza kujaza gesi na inapokwisha mfumo wa mafuta uka "pick" na kuendelea kuendesha gari bila ugumu wowote. Angalia picha zifuatazo zinazoonesha bi-fuel system.
Magari yanapotumia gesi inaweza kuwa "liquefied natural gas" (gesi ilihifadhiwa katika hali ya kimiminika) au "compressed natural gas" gesi asilia iliyo katika hali ya hewa. LNG "liquefied natural gas" inatoa nishati ya kuendesha gari sawa sawa na nishati inayoweza kutolewa na petroli. LNG inahitaji asilimia 30 tu ya nafasi katika tanki la CNG (compressed natural gas) ili kuhifadhi gesi kimiminika inayoweza kuzalisha nishati ya kuendeshea gari kama ile ya CNG. Kwa maana hiyo LNG inatumika kidogo kulinganisha na CNG kuzalisha nishati kubwa kuendesha gari. Ili LNG iwe ya baridi inahifadhiwa katika matanki yaliyo nje ya gari, Injini inapowashwa gesi inapashwa moto na kuwa katika hali ya kimiminika tena na kuanzia hapo mfumo unafanya kazi kama ule wa CNG.
Kumbuka:
Kituo chetu cha Songosongo kinajaza gesi aina ya CNG.
Ahsante kwa usomaji wako na alamsiki.
Kwa maoni, ushauri na maswali tuandikie katika sanduku la maoni au kupitia:
1. 0765749191
2. kitahsiyame@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni