Mpenzi msomaji wa bloggu yetu leo tutaangalia madhara ya kutumia rasilimali hii katika mazingira yetu na kwetu sisi wenyewe.
o Kwa mwili
wa binadamu ni sumu iwapo itavutwa (na
kuingia katika mfumo wa upumuaji wa binadamu). Ikivutwa kwa kiwango kidogo
haina tatizo. Ila ikivutwa kwa kiasi kikubwa kwa muda mrefu itasababisha
upungufu wa oksijeni mwilini hali inayoweza kupelekea kutokea kwa kizunguzungu,
uchovu, kichefuchefu na uhemaji usio mzuri kiafya.
Angalizo: Uwe makini unapotumia
vifaa vinavyotumia gesi asilia hasa majiko ya kupikia. Hakikisha
unapolitumia/usipolitumia hakuna uvujaji wa gesi kuepusha maafa.
o Rasilimali
hii ni rasilimali isiyokuwa na mbadala mara inapovunwa au kwa kiingereza tuna
sema ni “nonrenewable” energy source. Inapotumika haiwezi kufanywa tena kwa
matumizi mengine, hivyo basi tujue rasilimali hii inapochimbwa kiwango chake
kinazidi kupungua.
o Ni
rasilimali ambayo usafirishaji wake unagharama na una hitaji teknolojia ya juu
kwa sababu mara nyingi ni lazima isafirishwe katika mabomba (pipeline) na
kuwekea kemikali fulani za kusaidia usafirishaji salama.
o Pia gesi
asilia ina uwezo wa kulipuka/kuwaka na kusababisha maafa kama kuunguza nyumba
na samani na hata pia mwili wa mtu.
o Katika
kuitengeneza na kuitakasa rasilimali hii inapovunwa, kuna gesi ambazo pia
hupatikana kama mabaki ambazo si nzuri kwa afya ya binadamu zisipodhibitiwa
vizuri.
Haya
ni baadhi ya maafa mpaka sasa kutokana na kiwango chetu cha matumizi ya gesi.
Maafa yanaongezeka kutokana na kiwango cha matumizi na jinsi mfumo wa
usafirishaji gesi kwenye makazi ya watu ulivyojengwa ambapo kwa Tanzania sasa
bado hatujafikia kiwango hicho. Nchi zilizoendelea wana mifumo ya kupitisha
gesi kwenye makazi kama moja ya huduma za kijamii kama vile maji na umeme. Ni
mipango ya serikali hapo mbeleni kuwa suala hili litaingia katika mpango
mkakati wa kuutekeleza kama moja ya huduma ya kijamii kwa kila kaya japokuwa ni wa gharama kubwa sana.
Kwa maoni, ushauri na maboresho tafadhali wasiliana nasi kupitia sanduku la maoni hapo chini au
1. kitahsiyame@gmail.com au
2. kwa namba 0765749191
Ahsanteni na alamsiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni