Mpenzi msomaji habari yako?
Leo tutajifunza namna ambavyo rasilimali hii ya gesi asilia inavyochimbwa. Kwanza kabisa kijiografia gesi asilia inapakana na leya ya mafuta kwa chini na "shale" kwa juu ikifuatiwa na makaa ya mawe na miamba mengine juu yake zaidi.
Gesi ni matokeo ya mkandamizo na uozo wa viumbe hai (wanyama na mimea) iliyokufa miaka zaidi ya milioni iliyopita. Gesi asilia kikemikali ni methane CH4 lakini ndani yake kuna kemikali nyingine kama propane, ethane na hydrocarbon kubwa nyingine. Pia ina nitrogen kwa kiasi kidogo, kabonidayoksaidi, hydrogen sulphide na maji pia.
Mashine kubwa na za kisasa huingizwa ndani ya ardhi mpaka kule ambako rasilimali hii inapatikana ambapo inakuwa imechanganyikana na rasilimali nyinginezo. Sasa basi baada ya gesi kuchimbwa hupitishwa katika mitambo mingine ambayo huikausha na kuitengeneza tayari kwa ajili ya kuisafirisha katika mabomba (pipelines) kutoka machimboni kwenda maeneo yenye uhitaji kama Dar es Salaam.
Iwapo itasafirishwa kama ilivyo inaweza kuleta madhara kwa mabomba hayo ndio maana lazima iwe "treated" ili ifike salama. Na pia katika njia ya usafirishaji huwa kuna kuwepo na vituo mbali mbali ambavyo kazi yake ni kuongezea pressure kwa gesi inayosafiri ili mwendo wake usipungue njiani na kukwama. Vituo vyote hivi huwa vinasimamiwa na kompyuta na hata watu pia wakati mwingine kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa vituo hivyo pamoja na gesi inayosafiri.

Mpenzi msomaji, kitaalamu gesi asilia huwa haina harufu, lakini makampuni yanayochimba na kutengeneza gesi kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa watu huchanganya gesi hiyo na kemikali nyingine ambayo inaifanya iwe na harufu kama ya yai lililooza ili kusaidia kufanya utambuzi pale inapotokea ikavuja kuzuia maafa makubwa.
Kwa makala kama hizi usiache kufungua ukurasa wako kupitia kiungo hiki uhabarike zaidi https://oilinagesi.blogspot.com
Kwa maoni na ushauri usisahau kutuandikia kupitia sanduku la maoni hapo chini au kupitia
1. 0765749191
2. kitahsiyame@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni